Msanii wa Komedi, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji ameshindwa kutamba katika kura za maoni zilizolenga kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa kwa tiketi ya CCM.

Mchakato huo wa kura za maoni unatokana na kufariki kwa aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho, Deo Filikunjombe hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ililazimika kuarishwa uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo.

CCM imemtangaza Deo Ngalawa kuwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho akiwashinda wagombea wenzake tisa waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Deo Ngalawa alipata kura 537 akifuatiwa na mdogo wake marehemu Deo Filikunjombe aliyepata kura 501 huku Emmanuel Mgaya aliambulia kura 19.

 

Bartomeu Akiri Kumuhitaji Messi Game Ya Nov 21
Dkt. Slaa Atoa Tathmini ya Maamuzi Ya Rais Magufuli