Wataalam wa mambo ya siasa wanaamini kuwa hakuna uadui au urafiki wa kudumu katika siasa. Hicho ndicho kinachoanza kuonekana hivi karibuni ikiwa ni siku chache tu tangu kuanza kwa mikutano ya Bunge la Kumi na Moja.

Jana, varangati lisilofurahisha liliibuka Bungeni baada ya wabunge wa upinzani kupinga kwa nguvu tangazo lililotolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuwa Shirika la Habari Nchini (TBC) halitarusha Live vikao vyote vya Bunge.

Hata hivyo, varangati hilo lilionekana kuwaunganisha baadhi ya watu waliokuwa wakitajwa kama mahasimu, huku baadhi ya waliokuwa wakionekana kama marafiki kupitia vyama vyao wakitofautina.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alionekana kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi akicheka kwa furaha na kushikana mikono na Mwenyekiti wake wa zamani, Freeman Mbowe (Chadema) katika kikao na waandishi wa habari.

Zitto na Mbowe

Zitto ndiye aliyetoa hoja ya kupinga tamko la Nape na kuungwa mkono kwa nguvu na wabunge wote wa upinzani. Ikumbukwe kuwa Nape ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, alifukuzwa uanachama wa Chadema wakati wa Bunge la kumi.

Katika hatua nyingine, Picha zilizonaswa na waandishi wa habari, zinamuonesha Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe pamoja na Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea wakizozana na Waziri Nape.

Picha hiyo imepata umaarufu kwa kuwa Bashe alikuwa hasimu mkubwa wa Ukawa ingawa mwanzo alikuwa anamuunga mkono Edward Lowassa alipokuwa CCM. Wengi wanajiuliza kama Bashe amejiunga na upande wa Wapinzani katika mzozo huo wa TBC kutorusha ‘Live’ matangazo yote ya vikao vya Bunge.

Bado, haijafahamika moja kwa moja kama Bashe ameungana na Ukawa katika hilo, lakini sio wabunge wote wa vyama hukubaliana na kila kinachowekwa mezani na vyama vyao.

 

Waziri Mkuu amjibu Mbowe kuhusu ‘katazo kwa vyama vya siasa kufanya mikutano’ na TBC kutorusha Live Bunge
Serikali yawatetea Lowassa, Sumaye