Watu 15 wamejeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa kilimanjaro Mawezi baada ya basi la Kampuni ya Harambee kudaiwa kufeli breki na kuparamia magari mengine saba katikati ya Mji wa Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema ajali hiyo imetokea eneo la Benki ya NBC na majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya Mawenzi huku mmoja akiwa ndiye aliyeumia sana.

”Ni kweli ajali imetokea eneo la Benk ya NBC iliyopo katikati ya mji wa Moshi na kwasasa nipo Mawezi hospitalini ambapo majeruhi wapo 15 na mmoja ndiye aliyeumia sana lakini wengine wamepata majeraha madogo ya kawaida na mishtuko wanaendelea kupewa huduma ya kwanza” amesema kamanda.

Aidha, amebainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea na atatoa taarifa rasmi pindi utakapokamilika.

Tukio hilo la kuogofya limenaswa na kamera za CCTV likionesha namana basi hilo lilivyo shidwa kuzunguka katika mzunguko huo wa magari na kuparamaia magari saba kabla ya kusimama.

Serikali yautaka uongozi wa UDSM kuwachukulia hatua viongozi wa wanafunzi
LIVE CHATO: Rais Magufuli akizindua jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chato, Jengo la Jeshi la Zimamoto