Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako ameuagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuwachukulia hatua viongozi wa Serikali ya Wanafunzi ya Chuo hicho (DARUSO), walioipa Serikali saa 72 kulipa mikopo ya wanafunzi vinginevyo wataandamana.

Profesa Ndalichako alisema tamko hilo limetolewa kinyume cha utaratibu wa kutoa malalamiko na ni utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu ambacho hakiwezi kuvumilika, hivyo ametoa saa 24 kwa UDSM kuwachukulia hatua viongozi hao na apewe taarifa

Juzi DARUSO walitoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuhakikisha inatoa mikopo kwa wanafunzi waliokosa, vinginevyo watakutana nje ya ofisi za bodi hiyo

Ndalichako alisema kwa mujibu wa taratibu, Uongozi wa DARUSO unapaswa kuwasiliana na Mshauri wa Wanafunzi ambaye anachukua malalamiko yao na kuyapeleka kwa Makamu Mkuu wa chuo.

Aidha, alisema wanafunzi 45,000 wa mwaka wa kwanza, walipaswa kupewa mikopo, lakini Serikali imeongeza idadi na kufikia 49,485, na Tsh. bilioni 172 zimetolewa kwa ajili yao na wameshapata mikopo wote waliokidhi vigezo

Hata huvyo, Uongozi wa DARUSO umesema kauli hiyo ya Waziri ni ya dharau na wala haitawarudisha nyuma. Saa 72 zikifika watafika kwenye Ofisi ya Bodi ya Mikopo kama walivyopanga.

Video: Kibadeni airarua Simba, amshukia Matola kuhusu Sven, amwangukia Mo
Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi na kujeruhi 15