Klabu ya Bayern Munich imemteua aliyekuwa kocha wake wa zamani Jupp Heynckes kuwa kocha mpya wa klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu kufuatia kufukuzwa kwa Carlo Ancelotti.
Ancelotti alitimuliwa mapema mwezi Septemba kufuatia kupata matokeo yasioridhisha katika ligi ya Mabingwa na ikiwa katika nafasi ya tatu kwenye Bundesliga nyuma ya viongozi wa ligi Borussia Dortmund kwa pointi tano.
Heynckes mwenye umri wa miaka 72 amekuwa kocha wa Bayern mara tatu mara ya mwisho ikiwa 2013 wakati ambapo timu hiyo ilishinda kombe la vilabu bingwa, Bundelsiga na Kombe la Ujerumani kwa mara tatu.
”Bayern Munich iko moyoni mwangu, mimi na wafanyikazi wangu tutatumia kila njia ili kuleta tena mafanikio katika klabu hii niko tayari kukabiliana na changamoto hiyo” alisema Jupp Heynckes.
-
Syria yajisogeza fainali za kombe la dunia 2018
-
Andres Iniesta ajilipua FC Barcelona
-
Messi hatarini kukosa kombe la dunia 2018
Kocha huyo alitangaza kustaafu kujihusisha na soka mwaka 2013 ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Pep Guardiola lakini sasa anarejea na ataanza rasmi kibarua chake Jumatatu, na katika mchezo wake wa kwanza ataiogoza Bayern Munich itakapokaliana na SC Freiburg Jumamosi tarehe 14 mwezi huu.