Mkali wa ‘Sophia’, Ben Pol ametoa maelezo kuhusu tweet yake kwa Ali Kiba iliyozua utata na sintofahamu kwa mashabiki wa Bongo Flava.

Akiongea katika kipindi cha Friday Night Live cha East Afrika TV, Ben Pol alieleza kuwa tweet hiyo ilikwenda kwa umma kimakosa kwa kuwa yeye alipanga kuituma mojamoja kwa Ali Kiba kama ujumbe (Direct Message).

“Ni kitu ambacho kimenipa unyonge kidogo. Kwanza ile tweet haikuwa tweet ya public, ile tweet ilikuwa inaenda DM. Lakini kutokana na labda pilikapilika za kawaida… yani unaweza kuwa umetwet kitu umedhamiria kupeleka DM kumbe kitu kimeenda public halafu ukaingia kwenye mishemishe nyingine kama vikao, ukija kucheki unakuta ina likes 150, kuingia Insta nakuta watu wanaongea na ina comment zaidi ya 500… nafanyaje?” Alieleza Ben Pol.

Alieleza kuwa alishindwa kuifuta tweet hiyo kwa kuwa tayari imeshasambaa na kila mtu anaiona. Anasema alipanga kumtumia Ali Kiba DM kama sehemu ya maelezo ya utani kati ya msanii na msanii hata kama hawajakutana muda mrefu.

Jose Mourinho Kuinoa Manchester United, Mpango waiva
Ni Wapi Jose Mourinho Atakapo Jistiri?