Biashara United Mara wamejinasibu kuwa tayari kukabiliana na Young Africans katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC), utakaochezwa kesho Ijumaa (Juni 25), Uwanja wa Alli Hassan mwinyi Tabora.

Kocha Msaidizi wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu mjini Musoma mkoani Mara Omar Hamis, ameanika utayari wa kikosi chake kuelekea mchezo huo, alipozungumza na waandishi wa habari mjini Tabora leo Alhamis (Juni 24).

Kocha Omar Hamis amesema: “Lengo letu ni kuibuka na ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya Young Africans, na tumejipanga kufanya hivyo sababu kuingia fainali na kuchukua Ubingwa wa FA ilikuwa ni moja ya mkakati wetu kipindi ligi inaanza”

“Kila mchezo hua na approach yake, na approach itakayotumika katika mchezo wa kesho itakuwa tofauti na michezo mingine iliyopita tuliyokutana na Young Africans katika ligi kuu. Tuombe Mungu tuamke kesho tukiwa na Afya njema,”

Mchezo wa Nusu Fainali kati ya Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara umepangwa kuanza majira ya saa tisa na nusu alasiri, Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi, Tabora.

Nusu Fainali nyingine ya Michuano hiyo itacheza mjini Songea mkoani Ruvuma, Uwanja wa Majimaji kati ya Mabingwa watetezi Simba SC dhidi ya Azam FC.

ASFC: Historia ya Biashara Utd Vs Young Africans
Simon Msuva kulamba Milioni 18