Kocha wa zamani wa klabu ya Tottenham, Tim Sherwood amesema kama klabu hiyo inataka kubaki na mshambuliaji wake Harry Kane inatakiwa kushinda kombe msimu huu.
Kane amekuwa kwenye kiwango bora muda mrefu akiwa amefunga mabao zaidi ya 20 katika kila msimu kwa misimu mitatu iliyopita na tayari amefunga mabao 6 kwenye michezo yote aliyoichezea Tottenham msimu huu.
Pamoja na takwimu nzuri ya upachikaji wa mabao mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 bado hajashinda kombe lolote na hilo linawezakumfanya ahamie katika klabu nyingine kubwa zinazomuwinda barani Ulaya.
”Tottenham imekuwa klabu ya kiwangu cha juu na Harry Kane amekuwa katika kiwango bora kwa misimu kadhaa iliyopita lakini hiyo haitoshi kwani akiona vilabu kama Barcelona,Real Madrid na Manchester United vinamtaka ni rahisi kushawishika” alisema Tim Sherwood.
-
Karim Mostafa Benzema hadi 2021
-
Liverpool yatupwa nje michuano ya Carabao
-
Video: Messi apiga nne Barcelona ikiibamiza Eibar 6-1
”Njia peeke ya kumbakisha Kane ni kushinda walau kitu chochote msimu huu, kitu chochote sio kushinda kombe la Carabao bali kushinda ligi kuu au kombe la FA” aliongeza kocha huyo wa zamani wa Totteham.
Mwezi wa kumi na mbili mwaka jana Harry Kane alisaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia Tottenham mpaka mwaka 2022.