Serikali ya Sweden imeipatia Tanzania msaada wa sarafu ya nchi hiyo (SEK) milioni 450 sawa na shilingi bilioni 118 za kitanzania kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Emmanuel Tutuba na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Anders Sjöberg wamesaini hati za makubaliano za msaada huo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa mradi huo umelenga kuongeza fursa za kiuchumi na kijamii kwa kaya za walengwa pamoja na kulinda na kuimarisha rasilimali watu kwa kutoa ruzuku kwa kaya zilizoko kwenye mpango huo.

Hata hivyo hadi kufikia Desemba 2020 zaidi ya kaya milioni 1 zilihakikiwa Tanzania Bara na Zanzibar na kuingizwa katika mpango huo huku kaya 56,800 kazi ya kuzihakiki inaendelea ili nazo ziweze kuingizwa kwenye mpango huo ulioonesha mafanikio makubwa.

Mwezi Julai 2020 hadi Julai 2021, kaya za walengwa 871,654 zililipwa kiasi ha shilingi bilioni 171.8 kwa pande zote za Muungano na takwimu kuonesha kuwa ufukara ulipungua kwa asilimia 8 kwa walengwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF Ladislaus Mwamanga amesema kuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini umekuwa na manufaa na mafanikio makubwa.

Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Awamu ya Pili umeanza kutekelezwa mwaka 2020 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2023, umepangiwa kutekelezwa kwa gharama ya dola za Marekani milioni 883.3 sawa na shilingi trilioni 2.02 na Sweden imesaidia jumla ya dola na Marekani milioni 237 sawa na shilingi bilioni 542.2.

Simba SC yamuaga rasmi Luis Miquissone
Simba SC yaambulia sare ya pili Morocco