Kwa mara ya pili mfululizo Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, wameambulia matokeo ya sare katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki nchini Morocco.

Simba SC leo wamecheza mchezo wa pili wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Olympique Club de Khouribga.

Kiungo Mshambuliaji kutoka Senegal Pappe Ousman Sakho ameifungia Simba SC katika mchezo huo kipindi cha kwanza na wenyeji walisawazisha katika kipindi cha pili.

Sakho ameifungia Simba SC bao la pili tangu aliposajiliwa mwanzoni mwa mwezi huu, bao la kwanza alifunga kwenye mchezo uliopita dhidi ya FAR Rabat.

Simba SC imemaliza kambi ya nchini Morocco, inatarajia kurejea Tanzania mwishoni mwa juma hili.

Billioni 118 kunusuru kaya masikini mradi wa TASAF
Simba SC kurejea Dar