Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, kitarejea Dar es salaam mwishoni mwa juma hili kikitokea Morocco.

Kaimu Afisa Habari wa Simba SC Ezekiel Kamwaga amethibitisha taarifa za mpango wa kurudi nchini kwa kikosi chao ambacho kimeweka kambi kwa majuma mawili mjini Rabat, Morocco.

Kamwaga amesema baada ya kuwasili nchini wachezaji watapata mapumziko ya siku chache, kisha watarejea kambini katika moja ya nchi za bara la Afrika.

Hata hivyo Kamwaga hakutaka kuweka wazi nchi na mahala ambapo kikosi chao kitakwenda kuweka kambi ya kuendelea na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba SC yaambulia sare ya pili Morocco
Mlipuko wasikika nje ya uwanja wa ndege Kabul