Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imemkamata Maria Edson Mtambo (25) Mnyiha na mkazi wa Tegeta kwa Ndevu akiwa anasafirisha dawa za kulevya.

Binti huyo amekutwa na Dawa aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 448.1 akiwa na mpango wa harakuelekea nchini India, dawa hizo alizihifadhi katika kifurushi cha vitabu viwili ambavyo ndani yake kuliwekwa unga wa dawa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema kuwa binti huyo ni mfanya usafi huko Tegeta na aliyekuwa anamtumia dawa hizo ni mpenzi wake raia wa nje.

Kaji amewataka vijana kuwa makini na raia wa nchi za Magharibi kwa usalama zaidi.

Bofya hapa…..

Wafanyakazi KNH wagoma
Google yapiga panga App 17

Comments

comments