Mahakama mjini Barcelona nchini Hispania, imetaka kufanyika kwa uchunguzi wa mwili wa aliyekuwa rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos.
Kiongozi huyo wa zamani, alifariki katika jiji la Barlcelona Julai 8, 2022, akiwa nchini humo kwa matibabu.
Mahakama hiyo imeridhia kufanyika kwa chunguzi wa maiti hiyo, kufuatia binti Hayati Dos Santos, Tchize dos Santos kuomba kufanyika kwa uchunguzi wa mwili wa baba yake.
Mlipuko waua saba mpakani, Jeshi lasema linafuatilia
Binti huyo, ameonesha wasiwasi kuwa huenda kuna njama ya kumuua baba yake, ili kumzuia kuunga mkono upinzani katika uchaguzi ujao wa Angola.
Mawakili wa familia ya Dos Santos, wameshutumu hatua za serikali ya Angola kurudisha mwili wa marehemu Angola kwa mazishi ya kitaifa, ikiwa ni kinyume na matakwa ya rais huyo wa zamani ya kuzikwa kwa faragha nchini Uhispania.
Dos Santos alikuwa rais wa Angola kwa karibu miaka 40, akiongoza hadi mwaka 2017, na amefariki akiwa na umri wa miaka 79 kutokana na maradhi ambayo hayakuwekwa wazi.
Vyama vya upinzania kunda Serikali mpya
Taarifa ya rais wa Angola, João Lourenço imesema Dos Santos amekuwa akiugua ugonjwa wa muda mrefu huku Rais huyo akidai kuwa anaheshimu mchango wa Kiongozi huyo wakati wa uhai wake akisema alitawala kwa uwazi na ubinadamu.