Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka (TFF) imezipongeza timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara kuwa ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio.

Bodi hiyo imezifahamisha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 kuwa mchakato wa wa utengenezaji kanuni umeanza.

Bodi ya Ligi kwa sasa inakaribisha maoni, mapendekezo, marekebisho kutoka klabu ili kuboresha uendeshaji wa ligi. Maoni hayo yanapokelewa kwa njia ya maandishi moja kwa moja kwenye ofisi za bodi au kwa njia ya barua pepe tplb.tplb@yahoo.com

Joseph Odartei Kuchezesha Game Ya Young Africans Vs Sagrada Esperanca
MAJALIWA:WANAVYUO WAFUATE TARATIBU NA SHERIA ZILIZOPO VYUONI