Timu ya taifa ya Brazil imefanikiwa kunyakua ubingwa wa Olimpiki 2020 upande wa soka, kwa kuifunga Hispania mabao 2-1.

Michuano hiyo inayofanyika mjini kwa Tokyo-Japan ilishuhudia timu hizo zikifungana bao 1-1 ndani ya dakika 90, na kuongeza muda wa nyongeza (Dakika 30), ambapo Brazil walipata bao la ushindi katika mchezo huo.

Brazil imetwaa medali ya dhahabu kwa mara ya pili mfululizo kwenye michuano ya Olimpiki, wakitangulia kufanya hivyo mwaka 2016 mjini Rio de Janairo-Brazil.

Kocha Bbosa aipiga kijembe Young Africans
Young Africans yatupwa nje Kagame Cup