Baada ya kuiadhibu Young Africans katika mchezo wa mwisho wa Kundi A, katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Kocha Mkuu wa Express FC ya Uganda Richard Wasswa Bbosa, amewapiga kijembe Wananchi.

Express FC imetinga Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa kuibanjua Young Africans mabao 3-1, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha Richard Wasswa Bbosa, amesema alifahamu kikosi chake kinakwenda kushinda mchezo dhidi ya Young Africans leo Jumamosi (Agosti 07), kutokana na klabu yake kuwa na sifa ya ukubwa kuliko wenyeji.

” Express FC ni klabu kubwa kuliko Young Africans.” amesema Kocha
Richard Wasswa Bbosa, alipozungumza na Wanahabari.

Express FC na Nyasa Big Bullets zimekata tiketi ya kucheza Nusu Fainali ya Kombe la Kagame huku zikisubiri washiriki wawili kutoka Kundi B.

Ikumbukwe kuwa Express FC ndio mabingwa wa ligi kuu nchini uganda msimu wa 2020/21.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 8, 2021
PICHA: Brazil yatetea ubingwa Olimpiki