Msafara wa Waziri wa katiba na sheria , Harrison Mwakyembe umepata ajali eneo la Bwanga mkoani Geita ambapo gari la mkurugenzi wa mashitaka na makosa ya jinai limepinduka baada ya tairi la mbele kulia kupasuka.

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa na kukwepa watoto wawili waliovuka barabara bila tahadhari.

Hata hivyo katika ajali hiyo hakuna aliyepata madhara makubwa zaidi ya gari kupata uharibifu kidogo.

Waziri Mwakyembe yupo Mkoani Geita kikazi.

Video: Waziri Mpina Aiwashia Moto NEMC, Dawasco na Manispaa ya Kinondoni
Video: Waziri Nape Ayafutia Usajili Magazeti 473