Bunge la Iran limetenga dola nusu bilioni kwaajili ya kuboresha mradi wa silaha za nyuklia ili kuweza kujiweka sawa kiusalama dhidi ya maadui zake katika ukanda huo ambao umekuwa tishio kwa magaidi.

Iran imefikia hatua hiyo mara baada ya hivi karibuni kuwekewa vikwazo na Mrekani kuhusu mpango wake wa kuboresha silaha za nyuklia ambazo zimekuwa zikipingwa vikali na nchi hiyo.

Aidha, vyombo vya habari nchini Iran vimesema kuwa mpango huo unafanyika ili kupambana na vikundi mbalimbali vya kigaidi vinavyofadhiliwa na Marekani vilivyopo mashariki ya kati.

Hata hivyo, Makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani ikiwemo China, Urusi na Uingereza,, yameonekana kuwa kiwango kikubwa kama ndio suluhisho kubwa la kuzuia uundwaji wa silaha za nyuklia.

Raila atangaza kutoa ‘neno zito’, Polisi wanena kuhusu tuhuma za mauaji
Video: Mbowe akomaa na Rais Magufuli, Waziri alivyotua kiwandani kininja