Leo Mkaguzi wa Hesabu ya Serikali CAG, Mussa Assad ametoa msimamo wake juu ya kulitumia neno dhaifu na kusema kuwa wataendelea kulitumia neno hilo kulingana na taratibu za ukaguzi.
Ametoa kauli hiyo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ripoti ya mwaka unaoishia juni 2018, ambapo katika ripoti yake CAG ameonyesha matumizi ya neno dhaifu ikiwemo kutaja baadhi ya madhaifu katika vyama vya siasa na jeshi la polisi.
Ametaja udhaifu katika vyama vya siasa na kusema;
”Katika ukaguzi maalumu wa ununuzi wa sare za jeshi la polisi nilibaini kuwa jeshi la polisi Tanzania lilipa jumla ya shilingi bilioni 16 bila kuwepo ushahidi wa uagizaji na upokeaji wa sare za askari polisi kwa boharia kuu wa jeshi la polisi” amesema CAG.
Pia amezungumzia udhaifu katika vyama vya siasa na kusema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kilinunua gari jipya aina ya Nissan Patrol kwa shilingi milioni 147.76 ambalo lilisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya jina la bodi ya wadhamini na kuonyesha taarifa za fedha kama mkopo
“Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kilinunua gari jipya aina ya Nissan Patrol kwa shilingi milioni 147.76 ambalo lilisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya jina la bodi ya wadhamini na kuonyesha taarifa za fedha kama mkopo” Amesema CAG.
Pia, kwa upande wa CCM, CAG amesema, Chama cha Mapinduzi CCM hakikuwasilisha michango ya kila mwezi kwenda mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii NSSF.
Hivyo hadi kufikia Mei 2018 CCM ilikua inadaiwa shilingi Bilioni 3.74 pia hati za nyumba 199 zilizo Zanzibar zinazomilikiwa na CCM hati zake zimesajiliwa kwa majina ya maofisa na sio chama na sio bodi ya maofisa wa chama na sio bodi ya wadhamini” amesema CAG.
Aidha, siku chache zilizopita CAG alisema kuwa Bunge ni dhaifu kauli ambayo ilipelekea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Job Ndugai kuazimia kutofanya nae kazi.
Pamoja na msimamo huo wa Bunge, CAG aliendelea kusimamia kauli yake ya kuwa bunge ni dhaifu huku akisema kuwa neno dhaifu kitakwimu linamaanisha mapungufu na ataendelea kulitumia kama ambavyo amelitumia kwenye ripoti yake.