Katibu wa Siasa na Oganaizasheni, Jumuiya ya Wazazi Makao Makuu CCM Mkoa wa Iringa, Said King’eng’ena amewataka wazazi kushiriki katika vita dhidi ya vitendo vya ulawiti na ushoga vinavyoanza kuonekana kama vya kawaida katika baadhi ya jamii nchini.

Akizungumza katika kikao cha Baraza Kuu la jumuiya ya Mkoa huo, King’eng’ena amesema vitendo hivyo ni moja ya changamoto zinazotakiwa kushughulikiwa na Jumuiya ya Wazazi, ambayo inajukumu la kulinda malezi ya watoto na jamii kwa ujumla.

King’eng’ena, aliwataka wazazi kuongeza ulinzi zaidi kwa watoto wa kiume ambao wako hatarini kuharibiwa kizazi chao na kutengeneza kizazi kisichoeleweka katika nchi hii.

Katibu wa Siasa na Oganaizasheni Jumuiya ya Wazazi Makao Makuu, Said King’eng’ena.

Amesema, ” Nawaomba wazazi muongeze ulinzi kwa mtoto wa kiume kwa sababu mtoto huyu akifanyiwa kitendo hicho hawezi kuacha ataendelea kudai kufanyiwa au kufanya kutokana na mfumo wa maumbile ya huko nyuma, hivyo tuwalinde sana na kuwaepusha na vitendo hivi vya ulawiti.”

Aidha, amesema kuwa maadili na malezi katika familia nyingi yamepungua kutokana na wazazi wengi kuachia majukumu kwa wadada wa kazi jambo ambalo si jema kwa upande wa malezi kwa sababu watoto wengi wanafanyiwa ukatili na kukosa sehemu ya kusemea kutokana na wazazi kutokuwa na muda wa kuwasikiliza na kuwafatilia watoto wao.

DRC yashangaa shambulizi la Rwanda licha ya ujio wa Papa
Arsenal yaipandia dau Chelsea