Baraza la vijana Chadema (BAVICHA) limetishia kuitisha mgomo wa wanafunzi nchi nzima kwa mtindo waliodai ni wa kipekee usioleta madhara kwa taifa, endapo serikali kupitia bodi ya mkopo haitawapa wanafunzi wa vyuo mikopo ndani ya saa 72.

Bavicha limeeleza hayo jana wakati ambapo kuna malalamiko ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaodai kuwa bado hawajapata mikopo walioyoitarajia kutoka kwenye bodi ya mikopo nchini.

“Watueleze kwa kina, sio suala la kutuambia eti Bodi inasema kwamba itaenda kuzungumza na serikali ione namna gani ya kuongeza fedha. Kwa sababu sisi tunajua kwamba serikali hii ya CCM inazo fedha za kutosha za kuweza kuwalipia wanafunzi wa vyuo vikuu mikopo yao kwa kiwango kile ambacho kimeandikwa kwenye sheria,”alisema Katibu Mkuu Bavicha, Julius Mwita.

“Ikipita saa 72 sisi tutaingia kwa mfumo tofauti kuwaunganisha vijana wote wa chuo kikuu nchi nzima kwa sababu Bavicha imeenea nchi nzima. Tutawaunganisha vijana na watafanya mgomo wa aina tofauti usiokuwa na madhara wala ambao serikali haitajua umefanyikaji lakini wataona mgomo umefanyika,” aliongeza.

Hata hivyo, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini ilitoa ufafanuzi kuhusu kucheleweshwa kwa mikopo ya baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu na kukanuha taarifa kuwa wanafunzi hao hawatapewa mikopo.

Afisa Hbari wa Bodi ya Mikopo, Omega Ngole alieleza kuwa Bodi hiyo imetoa mikopo kwa awamu ya kwanza ambayo imewafikia wanafunzi 12,000 nchini na kwamba itaendelea kutoa mikopo kwa awamu nyingine hadi wanafunzi wote wanaostahili watapata.

“Hii Bodi ilianzishwa ili kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji wapate elimu ya juu na sio kuwafanya wasipate elimu ya juu.

“Kwa hiyo tunasisitiza tena tuliyotoa ni ya awamu ya kwanza, kwa kiingereza ni Lot 1, wanafunzi zaidi ya 12,000. Tunakanusha zile taarifa zilizosambaa kwenye mitandao kwamba Bodi haitatoa mikopo,” alisema Ngole.

 

 

Masikini Moyes, Kufutwa Kazi Wakati Wowote
Mmiliki Wa Chelsea Amfungia Vioo Jose Mourinho