Klabu ya Chelsea imetinga katika hatua ya robo fainali ya kombe la Carabao Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Everton.
Chelsea walitawala mchezo kwa urahisi katika kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungawa na Antonio Rudigers dakika ya 26 kabla ya Willian kufunga bao la pili wakati bao la kufuta machozi la Everton likifungwa na Dominic Calvert-Lewin.
Kocha wa muda wa Everton David Unsworth amesema kuwa timu yake ilimfurahisha licha ya kutolewa katika mechi ya kuwania kombe la Carabao dhidi ya Chelsea.
-
Samatta amaliza ukame wa mabao
-
David Unsworth atamani kuwa kocha mkuu Everton
-
Ronald Koeman atoa neno la shukurani, aiombea kheri Everton
”Nimepoteza mchezo huu lakini ninafurahia mchezo wetu, tuliwatawala mchezo kwa asilimia kubwa,” alisema Unsworth aliyechukua nafasi ya Ronald Koeman aliyetimuliwa na klabu hiyo.
Katika mchezo mwingine Tottenhama wakicheza katika uwanaja wa Wembley wamekubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa West Ham United huku Andre Ayew aking’ara katika mchezo huo kwa kupachika mabao mawili.
Moussa Sissoko na Dele Alli walifunga mabao ya Toteenham huku bao la ushindi la Wast Ham likifungwa na Angelo Obinze Ogbonna dakika ya 70.