Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayekipiga katika klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta alifunga bao moja wakati timu yake ikipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Club Brugge kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Luminus Arena jana usiku.

Samatta alifunga goli lake dakika ya 90 na kumaliza wimbi la kucheza bila kufunga ambapo alishacheza mechi tisa pasipo kufunga bao.

Bao la kwanza la Genk lilifungwa na Ruslan Malinovsky dakika ya 43 kipindi cha kwanza kabla ya Samataa kupachika bao la pili na kuifanya Genk kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Club Brugge.

Samata alijiunga na klabu ya Genk mwaka 2016 na kusaini kataba wa miaka minne kuitumika klabu hiyo akitokea TP Mazembe .

 

Odinga: Huo sio uchaguzi, ni maonyesho ya Jubilee
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 26, 2017