Serikali imewataka wananchi waliovamia kwenye maeneo ya reli kuondoka ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge).

Akizungumza na Uongozi wa Shirika la Reli (TRL) na Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli nchini (RAHCO) jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano kwa kuondoka kwa hiari,  ili serikali iweze kuanza ujenzi sambamba na kufufua njia za reli zilizo haribika.

“Miaka 15 iliyopita treni ya Tanga na Arusha haipo, serikali imedhamiria kurejesha kwenye nafasi yake, wananchi watupe ushirikiano. Serikali inataka kufufua reli zilizoyumba. Barabara zilikuwa hazimudu sababu ya kupitisha mizigo mizito. Serikali kupitia wizara ya Ardhi na TAMISEMI itawachukulia hatua watumishi waliohusika kuruhusu wananchi kujenga maeneo ya reli.” ameongeza

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu TRL, Masanja Kadogosa amesema shirika hilo limepanga kuanza ukarabati wa reli ya Arusha ambapo serikali imetenga zaidi ya bilioni 14 kwa ajili ya ujenzi huo, na kwamba imeshaanza kutia alama ya X nyumba zilizojengwa katika maeneo ya reli, mkoani humo

Chelsea yatinga robo fainali Carabao Cup, Tottenham yashindwa kutamba nyumbani
Video: Giza nene uchaguzi Kenya, Polisi kikaangoni