Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo hii leo Jumanne, Juni 20, 2023, amewasili Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kusikiliza changamoto za wananchi, kuimarisha uhai wa Chama pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Katika ziara hiyo, Chongolo ameongozana na Mjumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Ussi Gavu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa na watendaji wa Chama na Serikali.

Sanchez ampigia magoti Mikel Arteta
Young Africans yafunguka ishu ya Cedric Kaze