Shirika la Citizens for Responsibility and Ethics in Washington (Crew) la nchini Marekani limetangaza kuwasilisha kesi dhidi ya Rais Donald Trump kwa tuhumu za kukiuka marufuku iliyowekwa kwenye katiba dhidi ya kupokea malipo kutoka kwa serikali za nchi za nje.

Mawakili na watafiti wa shirikia hilo wanasema kuwa, Trump amekuwa akipokea malipo kutoka kwa Serikali za nje kupitia wageni kwenye hoteli zake na majumba yake ya kukodisha, hali sheria ya nchi hiyo inaharamisha malipo kama hayo.

Eric Trump, ambaye ni mtoto wa Rais Trump na makamu rais mtendaji wa shirika la Trump Organization ambalo linamiliki na kusimamia biashara za baba yake, ameekiita kitendo hicho kuwa ni usumbufu tu kwa nia ya kufaidi kisiasa, amesema kampuni ya Rais Trump imechukua hatua kubwa kufuata sheria kuzuia kesi.

Amesema kampuni hiyo imeahidi kutoa faida kutoka kwa hoteli zake ambazo zimetokana na wageni kutoka serikali za nje na kuziwasilisha kwa Hazina Kuu ya Marekani.

Aidha, Shirika hilo la Crew limesema litawasilisha kesi katika mahakama ya Manhattan, New York Jumatatu asubuhi.

Mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika hilo, Noah Bookbinder amesema kuwa shirika lake limelazimishwa kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya Rais Trump, kwani halikutaka kufikia maamuzi hayo kwakutumainia kuwa Rais Trump angechukua hatua nzuri za kuzuia kukiuka Katiba kabla ya kuingia madarakani. Tumelazimishwa kuchukua hatua za kisheria.

Jose Mourinho Amsemea Wayne Rooney
Arsene Wenger Aomba Radhi