Baada ya kuibuka tetesi kuhusu mshambuliaji wa Man Utd Wayne Rooney kuwa na mpango wa kuelekea nchini China, Jose Mourinho ameibuka na kusema hana tatizo na safari ya gwiji huyo endapo itatokea.

Mourinho amewaambia waandishi wa habari kuwa, suala la kuhama kwa mchezaji haliepukiki, lakini bado anaamini Rooney ana nafasi kubwa ya kuendelea kucheza soka katika ligi ya nchini England, hata kama ataondoka Old Trafford.

“Sipendi kupingana na maamuzi ya mchezaji yoyote kwa sababu hata mimi nafahamu faida na kuhaka kutoka mahala fulani kwenda kwingine … lakini mfano ni wa wazi kwa kila mmoja wetu anaependa soka, Zlatan (Ibrahimovic) mwishoni mwa msimu uliopita aliamua kwenda China ama the U.S.A?” Aliwahoji waandishi wa habari.

“Nafikiri jibu ni hapana, na ninafikiri hata kwa Wayne itakua hivyo hivyo, japo maamuzi yapo kwake na familia yake. Lakini bado ninaona kuna dalili za kuendelea kuwa hapa na kuisaidia timu yake.

Mwishoni mwa juma lililopita baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa, klabu ya Shanghai Shenhua ipo tayari kumsajili Wayne Rooney, baada ya kufanya hivyo kwa Tevez aliyesajiliwa kwa Euro milioni 84 (sawa na dola za kimarekani 89.66), huku Oscar akienda kwa wapinzani Shanghai SIPG akitokea Chelsea kwa Euro milioni 60.

Baada ya taarifa hizo, jioni Rooney aliisaidia timu yake kupata point moja kwa kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Stoke City na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na gwiji Bobby Charlton ya upachikaji wa mabao ndani ya klabu ya Man Utd.

Rooney alifikisha bao la 250 na kumuacha Bobby Charlton aliyeifungia Man Utd mabao 249 wakati akicheza soka.

Aristica Cioaba Kuisubiri Simba SC
Crew Marekani kumshtaki Trump, adaiwa kukiuka sheria