Mwanasoka Cristiano Ronaldo amevunja rekodi kwakuwa msakata kabumbu wa kwanza kushika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya Forbes ya walioingiza kiaisi kikubwa zaidi cha pesa kwa mwaka.

Forbes wamemtaja Cristiano Ronaldo kuwa mwanamichezo aliyeingiza pesa nyingi zaidi kwa mwaka 2016, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na bondia bingwa wa dunia, Floyd Mayweather mwaka 2015.

Kwa mujibu wa Forbes, Ronaldo aliingiza kiasi cha $88 million kama mshahara na ushindi alioupata. Pia, aliingiza kiasi cha $32 million kwenye ubalozi wa bidhaa mbalimbali na matangazo.

Ronaldo pia ameonesha ukubwa wake kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wafuasi zaidi ya milioni 215 kwenye Facebook, Instagram na Twitter.

Mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi ameshika nafasi ya pili katika orodha hiyo akiwa ameingiza kiasi cha $81 million.

Wawili hao wamechukua nafasi zilizokuwa zikishikiliwa na Floyd Mayweather na Manny Pacquiao mwaka jana, baada ya mabondia hao kutangaza kustaafu.

Video: Magazeti Leo Juni 10 - 2016
Audio: Simba imegonga mwamba kuinasa saini ya Kocha wa Zimbabwe