Mkuu wa wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili ameagiza baba mzazi wa watoto watatu, Meshack Michael kukamatwa kwa tuhuma za kuwadhalilisha kijinsia na kuwabaka mfululizo watoto wake huku akidaiwa kumpa ujauzito mmoja wapo.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wasamaria wema kutoa taarifa na kwamba vitendo hivyo vya udahalilisha vimekuwa vikifanywa na baba huyo kwa muda mrefu.

Aidha, Mkuu wa wilaya hiyo amevitaka vyombo vya uchunguzi kuharakisha usikilizaji wa kesi hiyo ili haki iweze kutendeka kwa watoto hao kwa wakati na iwapo mtuhumiwa akipatikana na hatia achukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.

”Nilishangaa kuona mwanangu aliye na umri wa miaka 13 akibeba ujauzito na tulipomuuliza alisema alikuwa akishiriki tendo la ndoa na baba yake mzazi kwa kumlazimisha wakati mimi nikiwa katika shughuli za uzalishaji mali,” amesema mama mzazi wa watoto hao Gaudenzia Meshack.

Naye Lucy John, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kupinga vitendo vya ukatili la Wadada Solution On Gender Based Violence la Jijini Mwanza amesema ofisi yake inafuatilia kwa karibu tukio hilo ambapo amesema limewaathiri kisaikolojia watoto husika.

Prof. Mbarawa, mama Mwantum waunga tela kinyang'anyiro urais Zanzibar
Visiwani Zanzibar wagombea urais wafika 9