Zoezi la kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais visiwani Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi linaendelea ambapo hadi kufikia sasa tayari wamejitokeza wanachama (9) tisa wa chama hicho kugombea nafasi hiyo.

Wagombea hao ni Shamsi Vuai Nahodha, Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Mbwana Bakari Juma, Balozi Ali Karume, Mbwana Yahaya Mwinyi, Omari Sheha Mussa, Shamsi Vuai Nahodha, Mohamed Jaffar Jumanne, Mohamed Hija Mohammed.

Zoezi la utoaji fomu rasmi lilianza June 16 katika Ofisi za Chama hicho zilizopo Kisiwandui Mjini Unguja na Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC, Idara ya organization Zanzibar, Cassian Galos Nyimbo.

Wanachama wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kugombea urais wakirithi nafasi ya Rais Dk. Mohammed Ali Shein, ambaye atamaliza muhula wake wa miaka 10 baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kukamilika Oktoba, 2020.

DC aagiza Baba aliyewabaka watoto wake watatu kukamatwa
Mkosamali ahamia CHADEMA, kugombea Ubunge Muhambwe "NCCR wamesinzia"