Muziki ni biashara kubwa hivi sasa na utamaduni wa wasanii wakubwa kuwasaini wasanii wenzao wakubwa Tanzania ulianzishwa na Diamond Platinumz baada ya kumsaini WCB msanii Rich Mavoko na sasa amemkaribisha mshindani wake mkuu, Ali Kiba.

Diamond amefungua milango kwa Ali Kiba leo kwenye kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm, baada ya mtangazaji wa Kipindi hicho Lil Ommy kuhoji kama anaweza kukubali kumsaini King Kiba kwenye label yake.

“No Problem, it’s all about business tu inawezekana… anakaribishwa,” alisema Diamond.

Katika hatua nyingine, Diamond ambaye amepangwa kutumbuiza kwenye jukwaa la MTV VMA mwaka huu akishare jukwaa hilo na wasanii wakubwa duniani pamoja na Ali Kiba, amesema kuwa itapendeza zaidi kama wote watapiga ‘show’ kali siku hiyo kwani wanaiwakilisha Tanzania.

Mdogo wa Ali Kiba, Abdu Kiba aliwahi kueleza kuwa yuko tayari kusaini WCB endapo watakubalina kibiashara na Diamond Platinumz.

Video: Ukawa wasema hawamtambui Prof. Lipumba, hawamtaki kwenye Umoja wao
Uganda wafanya mashindano ya ‘Miss & Mr HIV/AIDS’