Kazi ya Diamond Platinumz imeendelea kuonekana zaidi na kikubwa ni namna anavyoweza kuwachaguliwa mashabiki namna ya kulifuata baragumu analopuliza (ushawishi).

Jarida maarufu la ‘New Africa’ la jijini London Uingereza limemtaja mkali huyu wa ngololo katika orodha ya waafrika 100 wenye ushawishi zaidi kwa mwaka 2015.

Diamond New Africa

New Afrika imetaja sekta nane na watu wenye ushawishi zaidi katika sekta hizo ambapo Diamond ametajwa kwenye kipengele cha sanaa na burudani.

Vingele vingine ni Siasa, Michezo, Ofisi za Umma, Asasi za Kiraia, Teknolojia na Biashara.

Ni Magufuli Kila Kona Ya Afrika Mashariki, #WhatWouldMagufuliDo itakuvunja Mbavu
Serikali Yakata Mirija Mingine ya Matumizi