Tanzania imeibuka kidedea katika tuzo za Afrimma za mwaka huu zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, Dallas nchini Marekani, kwa kubeba tuzo tatu muhimu.

Kwa mara ya kwanza, Tanzania imeinyakua tuzo ya aina yake ya mchezea santuli bora barani Afrika, baada ya DJ- D Ommy wa Clouds Fm kupenya na kutajwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo.

Diamond Platinumz ameendeleza wimbi la ushindi wa tuzo kwa kutwaa tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki huku Harmonize akiondoka na tuzo ya msanii bora chipukizi.

“Team Tanzania, Mungu ni mwema siku zote,” Harmonize ameandika Instagram baada ya kupata tuzo hiyo.

Trump ataka Clinton afanyiwe vipimo vya matumizi ya dawa kabla ya mdahalo
Mbwana Samatta atajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika