Nahodha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Mbwana Samatta anaendelea kupeta kwenye anga za kimataifa ambapo sasa ametajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora Afrika inayotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kwa mujibu wa majina yaliyowekwa kwenye mtandao wa CAF leo, mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji atachuana na wachezaji 30 katika kipengele hicho.

Moto wa Samatta ulionekana tangu akiwa na klabu ya TP Mazembe mwaka jana alipoifungia magoli matano katika awamu ya robo fainali ambayo yaliiwezesha klabu hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kutua kwa mara ya kwanza katika fainali ya Kombe la Klabu bingwa Afrika, tangu mwaka 2010.

Mchango wa Samatta ulionekana pia ulionekana Taifa Stars baada ya kuisaidia kufika katika raundi ya pili ya mechi za kufuzu kucheza Kombe la Dunia. Hivi sasa ni tegemeo kubwa la Genk katika kupachika magoli.

Haya ni majina ya wachezaji wanaominyana na Samatta kubeba tuzo hiyo:

cafcaf-3

Diamond, DJ-D Ommy, Harmonize washinda tuzo za Afrimma 2016
Dongo la Rais Buhari kwa mkewe mbele ya Chancellor wa Ujerumani ‘lafufua makaburi’