Kauli tata ya Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari dhidi ya mkewe aliyedai hatamuunga mkono kwenye uchaguzi ujao imemuamsha mke wa rais mstaafu wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan, Mama Patience.

Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan na mkewe Mama Patience

Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan na mkewe Mama Patience

Rais Buhari aliyekuwa amesimama pembeni ya mmoja kati ya viongozi shupavu wanawake duniani, Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani, hivi karibuni wakati wakizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni nchini humo, alisema kuwa mkewe ni wa jikoni kwake na vyumbani kwake.

”Sijui ni chama gani ambacho mke wangu yupo, lakini ni mtu wa jikoni na sebuleni kwangu na vyumba vingine,” alisema Rais Buhari, kauli iliyomfanya Chancellor Makel kumuangalia kwa mshangao.

Mama Patience ambaye ni mwanaharakati wa kutetea wanawake na anayepinga wanawake kuchukuliwa kama wapishi na wafanyakazi wa ndani, ameibuka tena na kupinga kauli hiyo ya Rais Buhari akiwataka wanawake nchini Nigeria kuipinga kwa vitendo.

Kauli hiyo ya Rais Buhari dhidi ya mkewe, imeonekana kama inarudisha nyuma harakati za Mama Patience (Mke wa Johathan) za mwaka 2014, alipowaamsha wanawake kuacha na masuala ya kukaa jikoni ili wajitokeze kuomba nafasi za uongozi na kutetea wanyonge.

”Wanawake hampaswi kurudi tena jikoni. Sio sehemu yetu kurudi tena jikoni. Tuna wanawake ambao wanaweza. Tunaweza kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Nigeria,” ilikuwa kauli ya Mama Patience.

Hata hivyo, msemaji wa Rais Buhari, Garba Shehu aliwaambia waandishi wa habari kuwa kauli hiyo ilikuwa sehemu ya utani tu.

”Rafiki zangu, hivi kiongozi hawezi kusema neno lenye ucheshi/utani? Rais alicheka kabla hajatamka alichosema.” alisema Shehu.

Mbwana Samatta atajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika
Fuvu la binadamu lakutwa ndani ya nyumba ya 'Mchungaji’