Polisi wamethibitisha kuwa wamemkamata mwanamke aliyetaka kuwania urais Rwanda, Diane Rwigara kwa tuhuma za kughushi nyaraka wakati akiwania urais mapema mwezi wa 8 huku familia yake ikituhumiwa kukwepa kodi.

Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio la kukamatwa kwa mwanasiasa huyo lililohusisha mapolisi 10 ambapo polisi hao walilazimika kuruka katika lango la nyumba ya mwanasiasa huyo na kumkamata mara baada ya kukataliwa kufunguliwa nyumbani hapo.

Diane Rwigara anaishi katika mtaa wa Kiyovu mjini Kigali ambapo yeye mama yake na dada yake walitiwa mbaroni.

Juhudi za BBC kumtafuta msemaji wa polisi ili kupata maelezo zaidi hazikufanikiwa,

wiki iliyopita polisi wa Rwanda walitangaza kufanya upekuzi katika makazi ya mwanasiasa huyo na kutangaza kuwa ni sehemu ya upelelezi wa mwanzo kuhusu mashtaka yanayomkabili.

Diane Rwigara alikataliwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mwezi wa 8 na baadae akaanzisha vuguvugu la kukosa utawala wan chi hiyo.

 

Odinga aigomea tarehe ya marudio ya uchaguzi
Dele Alli hatarini kuzikosa fainali za kombe la dunia 2018