Maandalizi kueleka mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara  kati ya Azam Fc na Mbeya City fc uliopangwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar, yamekamilika.

 Muda mfupi uliopita Ofisa habari, Dismas  Ten, ameudokeza mtandao huu kuwa City iko tayari kwa mchezo huo hasa baada ya siku mbili za mazoezi jijini hapa kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa.

“Hatuna shaka,maandalizi yamekamilika, hali za wachezaji ni nzuri kabisa hakuna aliye majeruhi,tumefanya mazoezi kwa siku mbili lengo likiwa kuzoea hali ya hewa na mazingira ya kucheza usiku, kila kitu kimekwenda sawa imani yetu kubwa tutaibuka na ushindi” Alisema.

Makamu Wa Rais Akutana Na Ujumbe Kutoka Kingdom Leadership Networks
Yaya Toure Apingana Na Pep Guardiola