Zikiwa zimebaki siku mbili dunia ipambwe na rangi za malavidavi na wekundu wa mahaba kuadhimisha siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’, DJ mahiri kwenye mashine, DJ D-Ommy wa Clouds Fm aka Mr. Washawasha ametoa zawadi nzito ya bure kwa wapendanao.

VALENTINE

Mchezea santuri huyo ambaye amekuwa akitoa mfululizo wa Mix kali kila Valentine tangu mwaka 2014, mwaka jana aliipakua ‘Valentine Heart Felt Vol. 2, na mwaka huu ameijaza zaidi ‘Valentine Heart Felt Vol. 3’ kwa ajili ya mashabiki wake.

“Nimekaa nikaipika vizuri Mixx hii kwa ajili y awapendanao na nasikia furaha zaidi nikiwa sehemu ya kuinogesha furaha ya mashabiki wangu wapendanao,” DJ D-Ommy aliiambia Dar24.

“Ukiwa home, njiani unarudi au unaenda kwenye mihangaiko, chuo- hoostel, peke yako au na Baby- Number One wako au na washkaji tu. Uki-download na kuskiza Mixx hi nakuahidi hautajutia hasa katika weekend hii ya Malavidavi na hata baadae,” aliongeza.

D-Ommy amekuwa DJ Mtanzania aliyeyakuna masikio ya mashabiki wengi nchini na nje ya mipaka ya  Tanzania, amekuwa akipata mialiko kwenye matukio makubwa katika nchi mbalimbali za Afrika kutokana na kazi yake nzuri.

Kati ya mialiko mikubwa aliyohi kupata ni pamoja na Afro Caribbean Beach Party, BahRain, NBAA All Stars Pre – Party nchini Afrika Kusini na Wakilisha East Afrika ya nchini Kenya.

Enjoy:

Siku 100 za Magufuli: Sumaye amwagia sifa, Tafiti zaonesha anavyokubalika
Picha: Hawa ndio wake 10 wa marais wa Afrika, wanaotajwa kuwa wazuri zaidi