Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameendelea kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambapo jana aliutembelea mradi wa ujenzi wa mji mpya wa kisasa unaoratibiwa na Kampuni ya mfanyabiashara maarufu nchini, Said Bakhresa.

Dkt Shein alijionea maendeleo ya mradi huo ulioko katika wilaya ya Magharibi unaotarajiwa kuwa na majumba zaidi ya 300 ya kisasa na mpangilio wa kuvutia ikiwa ni pamoja na eneo la ufukwe litakalowavutia wananchi kwenda kupumzika.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa, Said Bakhresa alimueleza rais Dkt Shein kuwa mradi huo unaochukua eneo la kilometa 6 utakuwa wa kisasa na wa kipekee na kwamba majengo yataanza kuonekana yakisimamishwa kuanzia mwezi ujao (Disemba).

Mji huo uliopewa jina la Satellite City unatarajiwa kuwa na barabara za kisasa na mpangilio wa majenzi ya mji wa kimataifa.

Rais aliwataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanautangaza vya kutosha kupitia vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii huku akitania kuwa wasitangaze ‘mengine pekee’.

“Yatangazeni haya, wananchi wajue, watu wajue na dunia ijue, kwenye mitandao muweke, msiweke yale mengine tu,” alisema Dk Shein.

Wabunge wakataa Milioni 90 za Mashangingi, wataka zaidi
Chadema, Baba Wa Marehemu Waenda Mahakamani Kudai Kuuaga Mwili Wa Mawazo