Wabunge wa Bunge la 11 wamadaiwa kuzigomea shilingi milioni 90 walizopewa na serikali kwa ajili ya kununua magari aina ya Toyota Landcruiser Hardtop maarufu kama ‘mashangingi’.

Taarifa zilizomnukuu mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe zimeeleza kuwa wabunge waliitwa na katibu wa Bunge hilo, Dk Kashililah na kuelezwa utaratibu ikiwa ni pamoja na sahiki zao. Katibu wa Bunge aliwaeleza wabunge hao kuwa wanapata magari ya shilingi bilioni 90 kiwango ambacho ni sawa na kile cha mwaka 2010 hali ambayo ilizua zogo.

Wabunge hao walihoji iweje bei ya gari hilo iwe sawa na ile ya mwaka 2010 wakati dola imepanda baada ya miaka mitano. Hivyo, wabunge hao wanataka wapewe milioni 130 ambayo ni thamani ya gari hilo iliyoko sokoni. Imeelezwa kuwa Katibu wabunge aliwataka kuwasilisha suala lao serikalini kwani yeye hana uwezo wa kulizungumzia.

Akizungumzia taarifa hizo, Dk Kashililah alieleza kuwa anachofahamu ni kwamba kiasi cha fedha zilizotolewa kwa wabunge mwaka 2010 ndicho kitakachotolewa mwaka huu.

Awali, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alieleza kuwa jukumu hilo liko mikononi mwa serikali na kwamba wao wananchofanya ni kutoa posho kwa wabunge kwa ajili ya utendaji.

“Sisi huwa tunawahudumia jimbo allowance (posho) kwa ajili ya mbunge na kununua mafuta ya gari,” alisema John Joel.

Wabunge hukopeshwa magari hayo na kulipa kiasi fulani cha fedha ambazo Katibu wa Bunge hilo hakukitaja na kiasi kingine hulipwa na serikali kupitia Wizara ya Fedha.

 

Mbunge Aamua kumuandikia Spika Barua Ili Asilipwe Posho Za Vikao Vya Bunge
Dk Shein aendelea Kukagua Miradi, Akagua Mji Mpya wa Kisasa Unaojengwa Zanzibar