Wakati baadhi ya wabunge wakidaiwa kugomea milioni 90 za kununua magari maarufu kama ‘mashangingi’ kwa Madai kuwa haitoshi, mbunge wa SingidaMagharibi Mashariki, Elibariki Kingu  amekataa kulipwa posho ya vikao vya Bunge.

Mheshimiwa Kungi ameeleza kuwa atawasilisha rasmi barua yake ya kukataa kulipwa posho ya vikao ambayo ni shilingi 300 kwa siku kwa sababu mshahara wake unamtosha.

Ilibariki Kingu akizungumza na wananchi wa jimbo la Singida Magharibi (Picha kutoka Maktaba)

Elibariki Kingu akizungumza na wananchi wa jimbo la Singida Magharibi (Picha kutoka Maktaba)

Kingu aliwashamgaa wabunge wanaodai pesa zaidi kwa ajili ya magari huku wananchi wakiwa katika hali ngumu kimaisha.

“Mimi ziwezi kuchukua posho kwa ajili ya vikao, ” alisisitiza mheshimiwa Kingu ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga.

Pia,  mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alisema hatachukua posho ya vikao vya Bunge ingawa yeye hakuzungumzia namna atakavyozikataa rasmi.

 

Magufuli Afuta Sherehe Za Uhuru za Disemba 9
Wabunge wakataa Milioni 90 za Mashangingi, wataka zaidi