Rais John Magufuli amepiga marufuku sherehe za kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania bara (Tanganyika) zilizokuwa zikifanyika kila Disemba 9.

Taarifa ya uamuzi huo wa rais imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambaye ameeleza kuwa rais ameagiza bajeti ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya kufanya sherehe hizo ihamishiwe katika shughuli nyingine za maendeleo.

Amesema kuwa Rais ameagiza Disemba 9 iwe siku maalum ya kufanya usafi nchi nzima ili kupambana na ugonjwa wa kipindupindu unaolikabili taifa.

 

CCM Washinda Tena Ubunge, Waongeza Idadi Mjengoni
Mbunge Aamua kumuandikia Spika Barua Ili Asilipwe Posho Za Vikao Vya Bunge