Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amewasihi watalii na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wanaokumbana na changamoto zinazosababishwa na watendaji wa serikali, watoe taarifa ili hatua zichukuliwa.

Dkt. Kijaji amesema hayo akichangia katika mjadala wa Uzinduzi wa Tanzania Royal Tour uliofanyika kwa njia ya mtandao na kusisitiza kwamba haiwezekani mtu mmoja akarudisha nyuma jitihada za maboresho yanayofanyika.

“Ni muhimu sana wanapokumbana na kadhia za aina hizo watueleze moja kwa moja, simu zetu ziko hewani muda wowote. Tuoneshe mfano kwa mtu mmoja tu ambaye anaturudisha nyuma katika maboresho ya biashara na uwekezaji,” amesema kijaji.

Kauli ya Dkt. Kijaji imekuja saa chache kuelekea uzinduzi wa filamu ya Royal Tour itakayozinduliwa nchini Marekani katika miji ya New York na Los Angeles.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi filamu hiyo itawafikia watu bilioni 1 duniani kote katika mwaka mmoja wa kuisambaza.

Kocha orlando aondoka Bongo shingo upande
Aliyefuga nyoka 124 nyumbani kwake auawa na nyoka