Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameziagiza Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Fedha kufuatilia kiini cha wafanyabiashara wa Tanzania kuhamia nje ya nchi kwa madai ya vikwazo vya kuichumi.

Mpango ameyasema hayo wakati akifungua maonesho ya Wakulima Nanenane ambayo kitaifa yananyika Mkoani Mbeya na kuzitaka wizara hizo, kufanyia kazi na kubaini sababu za wafayabiashara kutoka nchi zinazopakana na Tanzania kupitia mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, kuacha kutumia bandari ya Dar es Salaam.

”Mshirikiane kupitia TRA na bodi ya biashara ya nje muweze kubaini ukubwa na kiini cha wafanya biashara wa Tanzania katika mikoa ya mipaka kuhamishia biashara zao upande wa baadhi ya nchi jirani katika ukanda huu,” amesema Dkt. Mpango.

Amesema, “lakini pia nimeambiwa baadhia ya wafanyabiashara wa nchi jirani wanapitishia bidhaa katika nchi zingine jiarani badala ya moja kwa moja kutoka hapa Tanzania.”

Katika hatua nyingine Dkt. Mpango ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kuangalia upya sheria za kifedha, huku akiwaagiza maafisa ugani kote nchi kubaki katika maeneo yao ya kazi ili kuwasaidia wakulima na kuwafundisha mbinu za kilimo cha kisasa ili kuwakomboa.

Awali, Waziri wa Kilimo Hussen Bashe, amesema kuwa imeundwa kamati ambayo itapitia mfumo mzima ya ukopeshaji wa sekta ya kilimo, ambapo meeleza kuwa kamati hiyo itashughulika na kubadili sheria zinazosimamiwa na Benki Kuu ambazo hazifanani na kilimo cha nchi hii.

Shambulio ndege zisizo na rubani laua kiongozi wa Al Qaeda
Serikali yatoa tahadhari virusi vya Monkeypox