Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameitaka jamii na kila mwenye uwezo kuendelea kuwasaidia watu wenye uhitaji, hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akizungumza na makundi maalumu wakiwemo wazee, wajane, watoto yatima na wenye ulemavu, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Watoto wenye ulemavu wa ngozi akiwa amembeba Mtoto Atra Suleiman, baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi sadaka ya vyakula kwa Wananchi wa Makundi Maalum wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Amesema Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni mwezi wa upendo, ushirikiano na kusaidiana hasa kwa jamii zenye uhitaji zisaidiwe kwa kadri ya uwezo watu waliojaaliwa nao.
Akizungumza mbele ya Rais Dkt. Mwinyi, mmoja wa wananchi hao Jamila Boraafya (Mlemavu wa macho) alimshururu Rais Dk. Mwinyi kwa jitihada anayoichukua kuwafikia wananchi wake wa makundi yote.