Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametembelewa na Balozi wa Norway nchini, Elisabeth Jacobsen aliyefika Ikulu kumuaga baada ya kukamilisha kipindi chake cha miaka mitano akiiwakilisha nchi yake hapa Tanzania.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika hii leo Mei 11, 2023 Rais Mwinyi alishukuru uhusiano uliopo kati ya Norway na Zanzibar, katika sekta ya afya na nishati ya umeme na kumtakia heri Balozi huyo.
Balozi Elisabeth, baada ya kuhudumu Tanzania kwa muda wake uliopangwa sasa anarejea nchini kwake Norway akiwa mstaafu.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar, imeeleza kuwa Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Norway kwa jitihda zake za kuiunga mkono Tanzania ikiwemo Zanzibar kwenye mambo ya kimaendeleo.