Joto la Uspika wa Bunge la Kumi na Moja linazidi kupanda huku Kamati Kuu ya CCM ikikutana leo mjini Dodoma kufanya mchujo kati ya majina 21 ya makada wa chama hicho waliorejesha fomu za kugombea nafasi hiyo.

Wakati hayo yakiendelea, imebainika kuwa kati ya makada hao, Dkt. Emmanuel Nchimbi na aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la 10, Job Ndugai ni majina yanayopewa nafasi kubwa zaidi ya kuchaguliwa.

Taarifa zilizopatikana kupitia chanzo cha kuaminika zimeeleza kuwa majina ya wagombea hao yanapewa nafasi kubwa kutokana na misimamo yao katika kukitetea chama chao.

“Pamoja na watu wengi kujitokeza ila nafasi kubwa ipo ziadi kwa wagombea wawili, spika huenda akawa Ndugai kwa upande Ndugai au Dkt. Nchimbi, Naibu anayetajwa zaidi ni Zungu. Na hao ndio watakaopitishwa kama hakutatokea mabadilika,” chanzo cha kuaminika katika mfumo wa Bunge kilieleza.

Hata hivyo, wakati majina hayo yakitajwa, tayari vita ya makundi ya watu wanaowaunga mkono imeanza kupitia mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu wamedaiwa kuanza kusambaza propaganda za kuchafua upande mwingine ili kuondoa uwezekano wa kupewa nafasi zaidi.

Wakati hayo yakiendelea, mwenyekiti mwenza wa Vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Freeman Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema ameeleza kuwa watatangaza jina la mgombea wao atakayewania nafasi ya Uspika mapema iwezekanavyo na kwamba watamtoa mtu makini na mwenye sifa zinazostahili.

 

Alichokisema Lowassa kuhusu Mauaji ya Mwenyekiti wa Chadema Geita
Lowassa Kuibuka Na Mazito