Mkandarasi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ametakiwa kuongeza kasi ili ujenzi ukamilike kwa wakati katika mji wa serikali mtumba Jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa na Waziri Stergomena Tax katika ziara yake ya ukaguzi wa jengo hilo ambapo amesema kazi bado ni kubwa na kuwataka waongeze bidii zaidi.
”Nimetembelea hapa nimejionea kazi ilipofika kazi bado ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi ili mUNGU akijalia mwezi oktoba mwaka huu badala ya disemba ujenzi uwe umekamilika na tuone tunajipanga namna gani” amesema Dkt Tax.
Amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutatoa ahueni kwa watumishi wa wizara na kuwawezesha kuwa sehemu moja na hivyo kurahisisha utendaji wa kazi wa Wizara.
Ujenzi huo utagharimu bil. 22.9 ambazo zimetolewa na serikali ili kuziwezesha taasisi za serikali kuwa na kuwa na majengoya kudumu katika mji wa serikali.