Mgombea anayewania nafasi ya kubeba bendera ya Republican katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Rais, Donald Trump ameibua jingine baada ya kuwataka wananchi wa Marekani kutosa bidhaa za kampuni ya Apple.

Akiongea katiaka moja ya kampeni zake Kusini mwa Carolina, Trump amewaeleza wananchi kuigomea Apple kwa sababu wamekataa kusaidia FBI kuingilia na kupekuwa mawasiliano ya mtu aliyefanya mauaji kwa kuwashambulia watu kwa risasi huko Saint Bernardino.

“Apple wameamua kutotoa mawasiliano ya hiyo simu, sawa. Ninachofikiria mnapaswa kuigomea hadi muda ambao watatoa hiyo ‘security number’. Mnaionaje hiyo?” alihoji Trump.

Alisema kuwa kitendo cha Apple kukataa kutoa mawasiliano hayo, kimepelekea FBI kushindwa kuwapata watu wengine walioshiriki kwenye mauaji hayo.

 

Watani wa Jadi: Simba wajeruhiwa, Yanga wacheka na nyavu zao
Madee afunguka baada ya kumsikia Dogo Janja akimchana