Chelsea FC ipo tayari kutoa Pauni 70 milioni ili kumsajili Mshambuliaji wa Juventus, Dusan Vlahovic katika dirisha lijao la majira ya kiangazi.

Staa huyu mwenye umri wa miaka 23, anadaiwa kuwa ni miongoni mwa mahitaji ya kocha mpya wa matajiri hao wa Jiji la London, Mauricio Pochettino.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Serbia ambaye amejiunga na Juventus akitokea Fiorentina katika dirisha la majira ya baridi mwaka 2021, Msimu huu amefunga mabao 14 kwenye mechi 41 alizocheza.

Mbali ya Chelsea huduma ya Vlahovic inahitajika na Manchester United ambayo kwa sasa inajiandaa kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumsajili staa huyo.

Man United inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumpata kwa sababu Vlahovic mwenyewe anataka kutua Old Trafford kwa sababu timu hiyo itakayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaay mwakani jambo ambalo Chelsea haitashiriki.

Polisi yafafanua tukio aliyekufa kwa kujirusha toka Ghorofani
KMC FC yarejea Dar es salaam